Dunia nzima imehama na kwa kasi isyozuilika inazidi kuhama kuelekea katika Teknolojia ya Kisasa. Kilimo pia hakikuachwa nyuma. Hadi sasa kama katika mpango kazi wako wa kilimo haujajumuisha kipengere cha teknolojia katika kufanikisha mradi wako anza kufikiri upya.
Leo kuna wateja wengi
mitandaoni kuliko katika masoko makubwa kama Kariakoo. Afrika pamoja na changamoto zake nasi hatuko nyuma. Hapa ni kwa uchache tu juhudi zinaonyeshwa katika nchi mbalimbali.
AFRIKA KUSINI: NEDBANK imetenga zaidi ya 2 Billioni za kitanza nia kuunga mkono mapinduzi ya kiteknolojia na uvumbuzi katika kilimo.
KENYA, Kenya climate innovation center wanaompango wa kufanya mapinduzi ya kiteknolojia ya kilimo katika eneo lote la africa mashariki. Ikijielekeza katika matumizi bora ya teknolojia ili kuhakikisha mkulima unakuwa na ujuzi wa kutosha wa hali ya hewa na kuzalisha mazao kwa kiwango cha hali ya juu.
ZIMBABWE shirika la umoja wa mataifa FAO limeanzisha mradi wa E- Vocha au vocha za kielectroniki zitakazosaidia wakulima kupata vifaa na matawa ya mazao kirahisi na kwa haraka.
MALI, TANZANIA na KENYA
Shirika la kiteknolojia Kickstart Linasambaza pump ndogo za umwagiliaji za kiteknolojia ya kisasa kwa bei rahisi kwa wakulima wadogowadogo.
NIGERIA KASKAZINI pia hawako nyuma wanafanya mapinduzi kwa kutumia Mtandao wa mawasiliano ya simu. wanatariajia wakulima zaidi ya millioni mbili wawe wanamiliki simu maalumu zitakazokuwa zinatumiaka kubadilishana taarifa za msini za kilimo.
Hii ni mifano michache tu katika viwango vya kawaija jinsi mapinduzi ya kiteknolojia na mawasiliano yanabadilisha taswira nzima ya kilimo barani afrika. Kama mkulima unanafasi ya kuzama katika ulimwengu huu ili uongeze uzalishaji, mapato, pamoja na upatikana jia wa taarifa sahihi.
No comments:
Post a Comment