unapenda kuwa mgunduzi kwa kiwango gani?




Karibu kila kitu unachokiona au kukitumia ni matokeo ya mtu fulani mahali fulani kuamua kuwaza tofauti na kisha kuyaweka mawazo yake katika utendaji.

Katika ulimwengu wa sasa
wa taarifa, unanjia mbili za kupita. Moja uamue kutumia taarifa hizi kufanya mabadiliko  katika maisha yako au uamue kuwa msikilizaji na msomaji wa taarifa na kuwa na maarifa yakinadharia.

Je kila mtu anaweza kuwa  mvungunduzi/innovator

Mwenyezi Mungu alituumba wanadamu wote sawa. Na akatupa uwezo wa kubadili kile kinachotuzunguka kilete manufaa kwetu zaidi. Kila mwanadamu aijalishi ni Mzungu au Mwafrika amezaliwa na uwezo mkubwa wa kufanya vitu vikawa.

Hujachelewa

Ugunduzi unaanza mahala ulipo. siri kuwa kwa vijana ni kuuliza maswali mengi mazingira au vitu vinavyokuzunguka. Maswali hayo yatakufanya kuona tatizo au upungufu. Baadae utaanza kufikiri nini uafnye kutatua tatizo hili. Ndivyo wanasayansi wa zamani walivyofanuya maisha yao.


Galileo Galilei (Muitaliano alaiyegundua dunia inazunguka jua)aliwahi kusema baada ya kuonekana analeta mawazo na vitu ambavo ni tofauti na jamii inayomzunguka.

"Sidhani wala siamini kuwa Mungu aliyetupa uwezo wa kufikiri, Akili, utashi, na uwezo mkubwa wa kufanya vitu vikawa, anategemea tusitumie uwezo huu"


kwa nini hatufanyi wala hatujishughulishi na kufanya vitu tofauti?

1. Tunaamini hatuwezi na tunaona ni mzigo mzito sana kufanya tofauti na mazoea au jamii inavyochukulia mambo.

2. Taarifa nyingi zilizotuzinguka. Hatutaki kupitwa na kitu, kila taarifa michezo,burudani,siasa, matolea mapya ya mavazi, yawezekana nyingi ya taarifa hizi nyingi zinakufanya upoteze umakini wa kile ambacho unakifanya. Mfano unaweza kukuta unataka kuwa mkulima bora, lakini asilimia tisini ya taarifa unazozifuata na kusoma ni michezo, burudani au taaarifa zilizo nje ya kile unachotakamani kuwa. sisemi taarifa hazifai lakini tunatakiwa kutawala jinsi ya kutumua muda wetu. unaweza kupanga Muda maalumu wa mamo haya sio kila dakika.

3. Mitandao ka kijamii  ni mizuri lakini nidhamu ya hali ya juu inapaswa kutumiwa katika kuitawala na sio kuruhusu yenyewe kututawala. Panga muda maalumu na sio kila saa kila dakiki upo mitandaoni unafanya vitu visivyokuletea tija.

4. Wapo watu wanaamini katika mikosi, ukoo hauna historia ya kufanya jambo fulani, wazazi hawasema mimi si lolote, walimu waliniambia mimi sina akili wala uwezo wowote. Hii imesababisha watu kuishi chini ya uwezo wao. Hivi vyote sio kweli. Unawezo mkubwa wa kufanya vitu vingi kwa utofauti na ukabadilimaisha yako kabisa.

Mwisho
 Amua kufanya vitu kwa tofauti, kinyume na mazoea. Jenga tabia ya kujaribu na kuona matokeo. Usiruhusu kukatishwa tamaa kwa aina yoyote ile. Tumia muda mwingi kufikiri jinsi ya kutumia uwezo ulio  nao kufanya mambo badala ya kusubiri wazazi, jamii, magazeti, mitandao ikuchagulie nini cha kufanya.  Dunia isingekuwa hapa kama watu wote wangeamua kuishi maisha ya kawaida.

MiradiKwanza













No comments:

Post a Comment