FURSA: OBASANJO NA ALIKO DANGOTE WAUNGANA KUWASAIDIA VIJANA WAJASILIAMALI AFRIKA
Bilionea wa afrika Aliko Dangote mwenye biashara zake hadi nchini tanzania, ameamua kuungana na rais wa zamani wa nigeria Olusegoni Obasanjo katika kuwakwamua wajasiliamali afrika.
Kupitia Africa Entrepreneurship Program (AWP) wanampango wa kuwasaidia
vijana wa kiafrika kuendesha miradi, kutoa mafunzo ya kumiliki makampuni a kuendesha miradi mikubwa yakijasiliamali.
Wanasema afrika ni mahala ambapo kuna ongezeko kubwa la vijana na uhaba wa ajira. Vijana kutoka nchi mbalimbali watakaochaguliwa kujiunga na program hii ya AWP watajipatia fursa hii ya kipekee.
Tarehe 01 Disemba 2015 vijana watatu kati ya hao walio watakaofanikiwa na mradi huo, waliofanya vizuri zaidi watapata fursa ya kusoma mipango kazi yao katika hafra itakayofanyika LONDON mbele ya waekezaji wakubwa duniani.
Mkutano huu utaudhuriwa na Maraisi na mawaziri wa fedha wa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.
Ewe kijana mbunifu Tanzania au popote ulipo Africa mashariki. Fuatilia kwa karibu fursa hii.
MAHALA:
Central Hall Westminster in London, 1-2 December 2015.
MAELEZO ZAIDI
www.tgais.com
jaza fomu na maelezo yako hapa
http://www.tgais.com/new-african-entrpreneurship-programme/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment