Nyanya ikiwa imeharibiwa na mdudu huyu hatari
Tuta absoluta/ leaf miner
nyanya ikishambuliwa
Tuta absoluta almaarufu kama kanitangaze mikoa ya nyanda za juu kusini na EBOLA kwa mikoa ya kati kanda ya ziwa wanamuita kipepeo au barababu.
Tuta absoluta ni mdudu mgeni hapa nchini kwetu anayeshambulia mazao jamii ya solanaceae haya yanajumuisha nyanya, viazi mviringo na majani yaliyo katika kundi hili.
Kwa hapa chini kwetu
mdudu huyu alionekana kwa mara ya kwanza Arusha.
Baadae akaripotiwa Morogoro na kuendelea kwa sasa yuko nchi nzima
Ni mdudu ambaye yupo hataondoka kwa wale walioacha kulima nyanya inatakiwa wajipange kukabiliana nae ama sivyo wasilime nyanya.
Tuta absoluta anashambulia hatua zote za ukuaji wa nyanya kuanzia kwenye kitalu.
Mdudu huyu anafanana kidogo na leaf miner japo yeye anakula kila sehemu ya mmea tofauti na leaf miner anayeshambulia majani pekee.
Dalili kuu za mdudu kuwamo shambani
ni kuona majani yanakuwa kama yameungua ukitizama vyema utaona kuna uchafu wa rangi nyeusi waweza muona naye pia katika majani.
Anataga mayai mengi sana ambayo huwa chini ya majani na huonekana kuwa na rangi nyeupe
Katika hatua yake ya ukuaji analeta madhara pindi akiwa funza anapokuwa mdudu kamili huwa kipepeo ambapo katika muda huo kazi kubwa ni kuzaliana
Kwenye maeneo yenye joto kali sana ama baridi kali mdudu huyu hastahimili vyema sehemu hizo uzalianaji wake ni mdogo.
Wakati wa mvua hupunguza wingi wa mdudu huyu kwa kuwaua wale vipepeo na hivyo kupunguza kasi ya uzalianaji.
Kama nilivyokwisha sema anashambulia zaidi mimea jamii ya nyanya kuna taarifa toka Dodoma ameonekana kushambulia pia hoho.
NJIA ZA KUKABILIANA NAE
Kuna madawa mengi ambayo yanatoa matokea mazuri ukiyatumia lakini changamoto imekuwa ni bei na usugu ambao mdudu huyu anautengeneza.
Dawa ambazo mpaka sasa zimetoa matokeo mazuri juu ya mdudu huyu ni Virtako, Ampligo, tank mix ya match na dynamec, pegasus, trigard, belt, couragen, runners and evisect.
Unapokuwa unatumia dawa hizi jaribu kuzichanganya wakati wa upigaji kwa mfano ukipuliza pegasus mara nne sitisha kuitumia tena tumia virtako hii itasaidia wadudu kutotengeneza usugu.
Usitumia dawa za jamii moja kwa kufatana hapa namaanisha dawa zenye kufanana mode of action.
Katika dawa nilizotaja hapo juu isipokuwa evisect zingine zimeobesha matokeo mazuri kwenye funza ili hali evisect imeonyesha matokeo mazuri kwenye vipepeo.
Kupambana na tuta inatakiwa IPM means Integrated Pest Management ifatwe.
Katika IPM itakupasa kuwa na lures ambazo hutoa harufu ikavutia madume ya tuta wanapokuja unakuwa unetesha kwenye beseni la maji wanakufa hii itasaidia kupunguza uzalianaji wa tuta kwa sababu madume watakuwa wachache.
Lakini pia kuna lure nyingine ya kupuliza asubuhi sana hii huwafanya funza wote kuja juu ya majani hapa ukipiga dawa matokeo ni asilimia mia ya kumuua huyu mdudu.
Njia nyingine ya kumdhibiti ni kulima kwenye green house ama agronets ila hapa inahitaji umakini mkubwa akiingia madhara yake huwa makubwa na kwa muda mfupi.
Tuta absoluta anaweza teketeza shamba kwa muda mfupi sana kwa sasa ukienda sokoni nyanya nyingi utakuta zina alama nyeusi ama matundu hayo ni madhara ya tuta.
Naamini bei ya nyanya haitoshuka kwa muda mrefu ama itazidi kupanda na akiianza shambulia kwa sana viazi mviringo bei nayo itapanda.
Ukiwa na mtaji wa kutosha lima nyanya utapata bei nzuri japo gharama za uendeshaji nazo zitakuwa juu.
Thanks: Ujasiliamali forum group
No comments:
Post a Comment