Kutana Vijana Hawa chini ya miaka 30 AFRIKA, Mabillionea watarajiwa


 Mubarak Muyika (Photo credit: Osborne Macharia)
Mubarak Munyika
Miaka 20, Kenya

Yatima akiwa na miaka 10, Baada ya kupambana na ugumu wa elimu alipata ufadhili wa masomo chuo cha Havard. Kafungua makampuni ya IT, Anazo huduma za kimitandao zinazotumiwa na makampuni mengi kwa kufungia mahesabu, kutafuta masoko, n.k inaitwa Zag Apps.


Bheki Kunene (Photo credit: Jay Caboz)

Bheki Kunene
miaka 27, Africa Kusini

Kunene amewahi kutuhumiwa kwa kesi ya mauaji na kukaa jela miezi mitatu hadi muuaji halisi alipopatikana, Amewahi kupata ajali ya gari kugongana uso kwa uso  na kusababisha ufa katika fuvu la kichwa chake ila alipona baadae, Ametengeneza ajira tisa kupitia kampuni yake ya kutengeneza tovuti Mind Trix Media. Kampuni yake inafanya kazi na makampuni yenye majina makubwa Afrika kusini, Italia, Zimbambwe na Angola.

Affiong Williams (Photo credit: George Okwong)

Affiong Williams
29, Nigeria

Machi 2012 alianzisha Kampuni inaitwa Reelfruit, inayofanya kazi ya kuchakata/process, kupaki, matunda katika ubora wa juu. Matunda yaliyokaushwa, Vitafunwana midhaa aina ya karanga zimefurika katika zaidi ya maduka makubwa 80 Nigeria. Sasa anajiandaa bidhaa zake zienee katika mashirika mbalimbali ya ndege duniani.



Alain Nteff
Miaka 22, Cameroon

Alishtushwa na vifo vya watoto wadogo na wakina mama katika jamii yake. Akiwa na miaka 20 aliamua kutengeneza App ya simu mabinti wajawazito na wauguzi kuhesabu siku halisi ya kujifungua. App hiyo imeshapakuliwa/downloaded na watu zaidi ya 500 inatumiaka kwa simu zilizotendenezwa kienyeji. Hadi kufukia 2017 anamipango iwafikie wajawzito zaidi ya millioni saba barani afrika.



Clarisse Iribagiza
Miaka 26, RWANDA
mmiliki wa kampuni iitwayo  HeHe Labs

Ni msichana wa kutoka rwanda mwenye kampuni ambayo inatumia technolojia kuangalia ufanisi wa makampuni ya kiserikali na binafsi ili kuboresha utendaji kazi wao. Mwaka 2012 HeHe ambayo maana yake ni "wapi" kwa kiswahili ilikuwa na mapato ya $200,000 kwa mwaka.



Verone Mankou
Miaka 28, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mmiliki wa Kampuni iitwayo VMK
Huyu ndiye mwafrika wa kwanza kutengeneza simu ya mkononi inayoitwa ELikia.
Pia amevumbua Way -C tablet ambayo ni  iPad ya afrika. Kabla hajapokea $700,00 kutoka kwa serikali ya kongo kuendeleza mradi wake, alikuwa akijifadhili mwenyewe. Mabenki yalikataa kumfadhili kwa sababu walimuona mdogo alafu kachanganyikwa.


Steven Sembuya
Miaka 28, Uganda
Mmiliki wa Pink food Industries
Baada ya kupitia changamoto nyingi kwa kila alichokuwa anakifanya. Sembuya ni miongoni mwa ukoo wa kitajiri sana nchini uganda. Aliamua kutumia shamba la familia yao la ekali 700 na kupanda Cocoa. Hili ndilo shamba la cocoa kubwa kuluko yote afrika. Anatengeneza Chokleti na bidhaa za cocoa zinazouzwa ndani na nje ya uganda.


No comments:

Post a Comment