ANZA KIDOGO: MAPINDUZI YA KIJANI, ANZA SASA



Zipo simulizi nyingi za watu wengi waliofanikiwa katika Kilimo na ujasiliamali. Kuna somo kubwa la kujifunza kutoka kwa nchi ya india. Wao miaka ya sitini waliibuka na mpango mkubwa wa Maapinduzi ya Kijani ambao leo tutajifunza masomo ya kutujenga katika kilimo chetu.

WAZO 

Mapinduzi ya kijani yalianza miaka ya 1965 nchini india. Lengo lilikuwa ni kuzalisha mazao mengi kwa kutumia ubunifu, teknolojia za kisasa na matumizi ya mbegu bora. Changamoto za mvua na maji ndio zilisababisha wajikite katika kutegemea kilimo cha umwagiliaji. Walianza kidogo kwa kujikita katika zao la Ngano. 

FUNZO
Usisubiri hadi uwe umetatua matatizo yako yote ndpo uanze kilimo. Anza kidogo ukiwa na wazo kubwa. Mambo yanaweza kwenda ndivyo sivyo, lakini Jifunze ulipofeli songa mbele. Wkati wa mwanzo unaweza kukmbana na ugumu mkubwa ajabu, Lakini kuwa na mpango maalumu wa kuyapindua maisha yako kupitia kilimo kama wahindi utafanikiwa.


MAZINGIRA YA MRADI

Sehemu kubwa ya Nchi ilikuwa na uhaba wa maji, pia mvua ilikuwa sio ya kutegemewa. Serikali ya India Iliamua kujikita kwa kutengeneza mifereji ya maji kwa wakulima, Kufanya Tafiti ya mbegu zenye kutoa mazoa mengi. 

Tanzania pamoja na kukabiliwa na changamoto kubwa kama hizi, Bado tuna maeneo mengi ya kufanya uwekezaji huu wa umwagiliaji. Anza sasa Anza kidogo kidogo.

MATOKEO SIO YA HARAKA HARAKA.

Mwaka 1970 ndipo matokeo yalianza kuonekana. Wananchi wakaanza kuona uhalisia ndozo za viongozi wao. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuondokana na balaa la njaa nalo likaanza kufanikiwa.
Miaka ya 80, Maono yao yakaanza kuonekana. wakawa na uwezo wa kuwa na chakula cha kutosha kwa wakati wote na misimu yote.Mwaka 1990 india waliweza kuzalisha tani Million 76 ya ngano na wakavunja rekodi. 

Mapinduzi ni muhimu katika kila hatua ya mwanadamu.Kilimo kwako chaweza kuwa ni  kwa ajili ya kujikimu lakini unapaswa kuvuka hapo na kuwa na wazo kubwa sana la kukifanya kilimo kubadili maisha yako kabisa kiuchumi.

MAOTOKEO YA KUWEKEZA KWA MIPANGO


India Inabaki kuwa mzalishaji wa pili mkubwa wa ngano duniani. Pamoja na changamoto za ukame na magonjwa ya mimea uwezo wa india umebaki kuwa ni tani millioni 70  ya ngano kwa kila mwaka.
Mapinduzi haya yalipangwa miaka zaidi ya 40 iliyopita kwa lengo dogo la kupambana na njaa huku nyuma yake likiwepo lengo kubwa la kuifanya india kuwa mzalishaji mkubwa wa ngano duniani. Leo unaweza kuanza na heka moja hadi kumi kulingana na uwezo wako. lakini pamoja na lengo dogo la kujipatia mahitaji yako inapaswa kuwe na lengo kubwa la kufikia zaidi ya heka 1000.

MWISHO.



Kama serikali makini waliweza kuweka malengo ya muda mfupi, kati na mrefu. Wakaamua kuwekeza katika elimu ya kilimo ili kuzalisha zaidi, Teknolijia yenye kuleta mazao zaidi,  Hata wewe kama mtu binafsi inawezekana. Kama umeamua kujiingiza katika kilimo miguu yote, kubali changamoto, gharama. Kubali kutumia muda wako kujifunza kilimo bora, Weka Malengo Makubwa sana Ila anza kidogokidogo. Bila kukubali kukatishwa tamaa, kurudishwa nyuma,  mafanikio katika kilimo kwako yatakuwa ni hakika.

Toa maoni yako hapo chini

No comments:

Post a Comment