PLAN: Fuga kuku watano kienyeji upate 200 kwa miezi sita





Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike  wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana).
Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho  na mchanganyiko kamili wa viini lishe
vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, 
yaani;

wanga, protini, calcium, chumvichumvi,
madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini).
Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/
kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini
juu ya uchaguzi wa majogoo).

 
Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia
kwa kuwajengea viota ndani ya banda.

Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha
mahali hapo pana usalama wa kutosha (mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).

Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya
mayai unayotaka kuku wako walalie.
 Hii inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na
vifaranga majogoo na mayai madogomadogo mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike.
Acha kuwawekea mayai ya mviringo kama mpira!


Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/ waatamie kwa pamoja.

Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako. 

Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai  machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku
wako huku mayai mengine yakisubiri awamu
ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano,
 Kuku 5 x Mayai 12 =Mayai 60.


Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa
vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku walioatamia chakula chenye viini lishe vya
kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata moja.

 Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende
kufukuzana na panzi na vyakula majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayai
yao.

Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga kibanda kidogo ndani ya banda kubwa
ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi kubwa na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga
watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo. 
Baada ya kuku hao 5 kuangua vifaranga wako 60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea
vifaranga inapoanza. Elewa kuwa ili upate mafanikio haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea
vifaranga inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza, Unatakiwa kuondoa na kuchoma
moto/kufukia mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa banda lote ili kuepusha
magonjwa kama vile kuharisha, viroboto,
papasi nk.

 Hapo unaweza kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja kadri
wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga wa mwisho, yaani Yule wa 60 na kuwaweka katika
kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na kuwawekea mayai mengine mama zao (yale
15/18 kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie
tena kwa siku 21 hadi 24 zingine.

 Unapotoa kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia humfanya kuku Yule ashindwe kutoka kwenye mayai maana hana mtoto wa kulea.


Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia maana atasubiri kupata vifaranga na ndipo atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila wasiwasi. 

Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umejipatia vifaranga/kuku zaidi ya 100 ndani
ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa
kuwapa chakula cha kutosha, maji, majani ya makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate
vitamini na madini mengine muhimu kwa afya zao.

 Fanya hivyo hata watakapokuwa wametotoa na ukawanyang’anya vifaranga. Hii
itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya maana kuku wengi hunyonyoka manyoya
wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na
kisha wataanza kutaga tena na kuatamia kama mwanzo.


 NAMNA YA KULEA VIFARANGA.


Katika ulezi wa vifaranga kama kuku  utawanyang’anya vifaranga vyao utatakiwa
kuwajengea banda dogo (ndani ya banda   kubwa/uzio) ili uwawekee chanzo cha joto
kama taa/jiko la mkaa (kama ni sehemu/
majira ya baridi).

 Kama utatumia jiko la mkaa  unatakiwa kuacha kwanza hadi mkaa mweusi
uwake wote ndipo uweke bandani maana  mkaa ukitoa moshi unaweza kuathiri vifaranga
vyako.

Angalia namna ya kuweka jiko lako la mkaa juu kidogo ili vifaranga wasiungue.
Hakikisha taa yako haitoi moshi sana na  haivujishi mafuta. Pia uwe na akiba ya mafuta
ya taa ya kutosha.

 Usiweke mafuta mengi kwenye taa maana inaweza kulipuka
ikakuletea hasara. Vifaranga wasizidi 50 kwa
boksi 1. Hakikisha umewasha taa/jiko lako ndani ya boksi saa tatu au zaidi kabla ya
kuwaweka vifaranga ili chumba/boksi lipate
joto kabla ya vifaranga kuwasili. 

Njia hizi  zinahitaji uangalifu wa hali ya juu sana kwani
kuhatarisha/kuua vifaranga ni kuhatarisha maendeleo yako. Kama utaamua kutumia
umeme pia ni vizuri zaidi maana inapunguza
hatari zaidi.

Kwa hiyoa njia zote tatu unaweza kutumia jedwali lifuatalo ili kuweza kumeneji joto la
kibanda cha vifaranga;


UMRI WA KUKU/VIFARANGA JOTO NDANI YA BOX/KIBANDA  CHA KULELEA VIFARANGA JOTO NDANI YA CHUMBA/BANDA


Wiki 1 33-35oc 30-32oc
Wiki 2 30-33oc 27-29oc
Wiki 3 27-31c 24-26oc
Wiki 4 24-29oc 21-23oc
Wiki 5 26-27oc 22-23oc

Baada ya wiki ya 4/5 pasua box/watoe kwenye banda la kulelea ili walelewe kwa joto la
kawaida la banda/chumba.

Kwa kawaida joto hupimwa kwa kipimajoto (thermometer), lakini kama huna kipimo hiki,
njia rahisi ni kuwaangalia kulingana na tabia
zifuatazo;

 Kama vifaranga wamejikusanya sehemu moja basi joto ni kidogo bandani
mwao, 

au kama wanaenda mbali na chanzo cha joto huku wanatanua mabawa yao na
wakihema harakaharaka basi joto ni kali/  limezidi kiwango.

 Pale watakapo tawanyika
vizuri ndani ya boksi/kibanda cha kulelea
huku wanakula na kunywa maji vizuri basi
joto ni la wasta na ndilo linalofaa. Kama
unatumia njia ya Boksi, basi unatikiwa
kulipanua kulingana na ukuaji na mahitaji ya
vifaranga vyako.


Vifaranga wako wape chakula cha vifaranga cha kutosha, maji safi na salama, majani
mabichi ambayo hufungwa kwa kuning’inizwa kwa kamba,na CHANJO za minyoo nk ili
wapate vitamin, madini na protini itakiwayo na
kuzuia tabia ya kudonoana ili wakue vizuri.


Hakikisha kuwa chumba chao ni kisafi na hakina unyevunyevu wakati wote.
Unyevunyevu husababisha ugonjwa wa baridi na hufanya vifaranga wajikunyate na
kutetemeka na wanaweza kufa ghafla! Inashauriwa kuwa siyo salama kufuga aina
nyingine ya ndege kama vile njiwa, bata, bata
mzinga nk kwa kuwachanganya na kuku
maana kila aina ya ndege wanamagonjwa yao.



Hivyo kuwachanganya kutakufanya ushindwe namna ya kuwatibu wanapopatwa na ugonjwa.



Pia chawa wa njiwa huleta ugonjwa wa Ndui hasa kuku wanapoangua vifaranga wao.

 Hapa ugonjwa unaweza kufyeka vifaranga wako
wote 60/100 kama utafuata ushauri wangu!

Baada ya wiki 2 hadi 3 baada ya kuwanyang’anya vifaranga kuku wako
wataanza tena kutaga mayai. Wakiatamia wote 5 Kama utaimarisha huduma kwao na kwa
vifaranga/kuku wale 100 tayari utakuwa una
kuku 105 au zaidi. 


Kuku wale 5 wa mwanzo wakiatamia tena kwa siku 21 hadi 48 (kama
utafuata mfumo ule wa mwanzo wa
kuaatamishia mara 2) utajipatia vifaranga
wengine 100 tena na hivyo kuwa na kuku
zaidi ya 200 ndani ya miezi 5/6 tu!




Ukiwahudumia vifaranga wale wa mwanzo 100 vizuri kwa miezi 3 na nusu nao wataanza
kutaga kama mama zao. kwahiyo, Chukulia  walalie majike 5 wa mwanzo na majike 50 waliopatikana baada ya uzao wa kwanza kwa
miezi ile 3 ya mwanzo utakuwa na mitetea 55.


Wote wakiatamia na watoe vifaranga 10 kila
mmoja kwa siku zilezile 21 hadi 46, tayari
utakuwa na vifaranga 550! 


Sasa jumlisha na wale 150 waliobakia kati ya kuku 200 na wote
wakakua vizuri utapata kuku na vifaranga zaidi ya 700! Jumlisha na 550 watakaototolewa
na mama zao wale 5 wa kwanza na wale 50 wa uzao wa 1 na 2 kwa mara ya 2 si tayari
utakuwa na kuku zaidi ya 1,200 ndani ya miezi 6 hadi 8 tu? Hivyo utajikuta unao kuku
zaidi ya 1,000!

Kati ya kuku 1,000 ukisema utoe kuku 800 wa kuuza na ukiwauza kwa bei ya Tsh. 4,000 kwa  kila kuku 1 tayari utakuwa na Jumla ya Tsh.
320,000/= ambazo unaweza kufanya mtaji
wa mambo mengine au kuboresha mradi wako
zaidi. Unafikiri hapo hujaanza kufikia lengo la
kuku 1 akuletee shilingi Milioni 1?

 Ukiendelea hivi inamaana kuku 1 atakuzalishia zaidi ya hapo.



 BANDA LA KUKU.

Unatakiwa kuwa na banda bora la kufugia kuku ambalo litaweza kutunza kuku ili
wasiweze kupatwa na madhara mbalimbali kama vile; kuliwa/kujeruhiwa na wanyama
wakali, kuchukuliwa na wezi nk. 

Lakini banda bora pia litawasaidia kuku kuhimili mabadiliko
mbalimbali ya hali ya hewa yanayoweza kujitokeza.


Sehemu ambayo inafaa kwa ujenzi wa banda bora ni ile ambayo inaweza kufikika kwa
urahisi, iwe na mwanga wa kutosha, isiwe na upepo mkali na isiyoruhusu maji kusimama au
kuingia ndani.


Banda ni vema likawa la ukuta/mbao/ mabanzi.matete/mianzi imara ili lishikilie paa
vizuri lisianguke. Kuta hizi zaweza kujengwa kwa matofali ya saruji/matope/kuchomwa/
mabanzi/mbao nk. 

Katika kuezeka waweza kutumia mabati/vigae/nyasi. Banda ni vema
likawa kubwa kulingana na kiasi cha kuku na
umri walionao.

 Kitu cha kuzingatia ni kwamba
banda liwe na hewa ya kutosha.
Kuku wanaofugwa ndani ni vema
wakatengenezewa uzio mpana (angalau Mita
8x10) ili wapate mahali wanapoweza kuota jua,
kupumzikia/kupunga hewa na kufanya mazoezi
(wawekee kamba/bembea/ngazi ndani ya
banda). 

Hakikisha kuwa banda ni imara na  hawatoki nje ya banda na kwenda mbali ili
uweze kuwawekea chakula cha kutosha na  maji na hata wale wanaotaga/kuatamia
wapate chakula na kurudi haraka. 

Banda likiwa kubwa na bora litapunguza magonjwa kwani litakuwa na hewa ya kutosha
ambayo itasaidia kupunguza joto na unyevunyevu usio wa lazima bandani mwako.
Hii itasaidia uingizaji oksijeni ya kutosha na  kupunguza hewa chafu zenye madhara kwa
kuku. 

Pia litasaidia namna ya kufanya usafi kwa urahisi na kupunguza vumbi ambalo
linaweza kusababisha kikohozi kwa kuku wako. Ni vema banda lisipungue Mita 3 kwenda juu. Mambo muhimu ndani ya Banda.

1. Sakafu nzuri (iliyotengenezwa kwa saruji/
udongo ili isituamishe maji. Isiwe na nyufa
ili iweze kusafishwa kwa urahisi.


2. Hakikisha kuwa banda linakuwa na Viota
(vitagio) vizuri kwaajili ya kutagia. Viota
viwe na urefu wa Sentimita 30 na upana
sentimita 30 na kina sentimita 35. Sehemu
ya mbele izibwe kwa sentimita 10 tu chini.
Sehemu zote hizo zizibwe kwa ubao. Kama
kuku wako ni wakubwa unaweza kuongeza
upana, urefu na kina kiasi cha kutosha
mfano, Upana na Urefu 35cm, kina 55cm
nk. 

Hakikisha kiota/kitagio kinakuwa na giza kiasi maana kuku hupenda kutaga mahala
pa giza kidogo/palipojificha. Giza litasaidia kuku asiweze kula mayai au asiweze
kudonoana na kuku wengine. Kiota pia kinatakiwa kiwe mahali ambapo ni rahisi
kwa kuku kuingia na kutoka, pia iwe ni rahisi kusafisa.


Ndani ya kiota kuwekwe majani makavu/ maranda ya mbao laini na kinyunyize dawa ya
unga ya kuzuia viroboto/utitiri kabla ya kuweka nyasi.


AIDHA, ni vizuri sana kuwawekea kuku wanaoatamia mayai wakati wa usiku maana
ukimuwekea wakati wa mchana anaweza kuyaacha.


Kuku anayetarajiwa kuatamia ni vema akachunguzwa kama anao utitiri/viroboto/
chawa kwenye manyoya yake. Wadudu hawa humkosesha raha kuku anayeatamia na wengi huacha mayai na kukimbia/wasitulie kwenye
viota vyao.

 Hali inapelekea kuanguliwa kwa vifaranga wachache. Unaweza kumuona
mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi.


1. Banda liwe na vichanja maana kuku
hupenda kulala juu ya vichanja maana nao
ni ndege.

2. Vyombo safi na vizuri kwaajili ya chakula na
maji.

3. Walazie majani makavu/maranda ya mbao/
makapi ya mazao sakafuni kwa banda
zima.

thanks to wajasiliamali forum

No comments:

Post a Comment