Tanzania, Uturuki kuzidi kudumisha mahusiano ya kibiashara



Tanzania na nchi ya uturuki wanaendelea kuwa na uhusiano mzuri kibiashara. Hii ni baada ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na Turkish Foreign Economic Relation board (DEIK).

Lengo la kuboresha mahusiano haya ya
kibiashara ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa nchi hizi mbili pamoja ili kuweza kutumia kila fursa za kibiashara na uwekezaji zinazojitokeza.

Miongoni mwa manufaa ya kuboresha mahusiano kati ya nchi hizi mbili ni kama ifuatavyo.

1.kuongeza uwezo kwa watanzania kutafuta nafasi zaidi za kibiashara nchini uturuki kwa wepesi.

2. Kuwawezesha wawekezaji kutoka uturuki kuja kuwekeza nchini tanzania hivyo kutoa nafasi za ajira, masoko kwa bidhaa za ndani na maendeleo kiucumi.

3. Kubadilishana kwa ujuzi na uzoefu  wa kibiashara kwa wafanyabiashara wa nchi hizi mbili.

4. Kukua kwa uwekezaji katika sekta ya kilimo, maana nchi ya uturuki iko mbele kwa mbinu na teknolojia ya kilimo.

5. Makampuni ya uturuki yatazidisha kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu kitu ambacho ni muhimu kwa maendereo ya watanzania.

Ni wakati kwa watanzania kutumia fursa hii ya kibiashara.

miradi kwanza

No comments:

Post a Comment