Kilimo cha ZABIBU Bahi, TIB kuwezesha vikundi vya wakulima




Katika harakati za kujikomba kiuchumi, Miradi itakayosimamiwa kwa umakini wa hali ya juu pekee ndio njia itakayoweza kubadilisha maisha ya watu wenye kipato cha chini hususani wanavijiji.

Katika Wilaya ya Bahi Dodoma Tanzania,
Kupitia SACCOS benki ya uwekezaji tanzania |(TIB) inatarajia kuunga mkono jitihada za wananchi wa Bahi kujikomboa kiuchumi kwa kutoa mkopo wa zaidi ya Billioni 1.3 kwa wanakijiji wa Lamaiti.

wanakijiji hao pia wamepokea mkopo kutoka UTT Microfinance Millioni 275.

Fedha zote hizi ni kuwezesha wakulima wa zabibu wilayani hapo ili kuweza kutumia fulsa hii pekee ya kilimo katika eneo la zaidi ya hekta 170. Pia kwa ajili ya kusapoti ujengwaji wa kiwanda cha mvinyo ambacho kitaweza kutoa soko kwa zabibu zinazozalishwa na wananchi hao.

Huu ni mfano mzuri wa kuigwa katika vijiji vyote Tanzania. Kama kupitia Vikundi  kuandaa mchanganuo mzuri wa mradi unaokopesheka  uliojielekeza kutumia fursa zilizopo kijiji hapo maendeleo yatakuwa ni ya uhakika.


Kuanzisha mradi ni jambo moja jambo la muhimu zaidi ni kuwa na mbinu na elimu ya kutosha kutawala na kuendesha miradi ili tija ionekane.

miradi kwanza









No comments:

Post a Comment