Uganda nchi ya kwanza duniani kwa watu wengi kujiajiri/wajasiliamali.








Katika hali isotegemewa uganda nchi isiyo na bahari, yenye changamoto lukuki katika kila nyanja imeibuka na kuwa nchi namba moja duniani kwa kuwa na
watu wazima wengi waliojiajiri. Asilimia 28.1 ya waganda wamejiajiri takwimu ambayo haifikiwi na nchi yoyote duniani.


Katika historia ya ajira, wakati wa mapinduzi ya viwanda duniani watu waliona ni hatari zaidi kuajiliwa kuliko kujiajiri. Maana waliogopa kuwa ipo siku moja nitafukuzwa kazi kiwandani na familia yangu itateseka. Dunia ya sasa hasa afrika mahali palipojaa fursa za kila aina, pamoja na hatari ya kupoteza ajira, makampuni kupunguza wafanyakazi, mengine kufungwa, mengine kuajiri kwa muda tu, mengine kukufanyisha kazi hadi familia kuvunjika bado wengi tunaona ni bora tuajiriwe tu kuliko kujiajiri.


Kwa mara ya kwanza katika takwimu nchi ya afrika imezipiku mbali kabisa Marekani na Uingereza katika suala la watu kujiajili. Hili ni somo kwetu wengine tutambue fursa zilizotuzunguka na kuchukua maamuzi ya kuingia miguu yote miwili katika kujiajiri.



No comments:

Post a Comment