Utafiti unaonyesha 80% ya chakula kinacholiwa africa kinalimwa na wakulima wadogo wadogo. Uhamasishwaji wa kilimo ni vizuri uende moja kwa moja na
kuunganishwa kwa wakulima wadogo wadogo na Wenye viwanda. wakulima wadogo wadogo wamekuwa wakiangia mikononi mwa madalali na walanguzi bila kujua au kuwa na elimu ya kuthanimisha mazao yao.
Tunaishi katika zama za taarifa na nawasiliano. Wakulima wengi vijijini wako nyumba kabisa kwa hili la taarifa. Kumekuwepo na shimbo kubwa sana linalowatendanisha wakulima na wanaotumia bidhaa zao ambao mara nyingi ni wamiliki wa viwanda vikubwa na vya kati.
SOMO KUTOKA UGANDA.
Africa AgriBusiness Academy (AAA) uganda wamezindua mfumo wa kuwaunganisha moja kwa moja wakulima wadogo wadogo na wamiliki wa viwanda. Hii itasaidia maelfu ya wakulima kukutana na wanunuzi halisi wa bidhaa zao pia kuboresha sekta hii.
No comments:
Post a Comment