Soma Hapa Fursa Mradi wa Kuku Kibaha






Shiriki la Elimu Kibaha limeingia ubia na kampuni ya Organia toka Egypt na Turkey kwa ajili kuzalisha na kuuza kuku walio katika ubora wa masoko ya Ulaya, lengo likiwa ni kuzalisha na kuuza kuku milioni 3 kwa mwaka huku 80% Ikiwa exported na 20% soko la ndani. lakini kukamilika kwa mradi huu watafikia uwezo wa kuzalisha  kuku Millioni 165 kwa mwaka. 


Katika makubaliano hayo, kuna nafasi kuu 3 kwa ajili ya wawekezaji wa ndani:

1) Kampuni itanunua raw materials kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku ambayo 65% ni yellow maize, 25% Ikiwa ni soya beans na 10% other nutrients.  Wanahitaji 8,000 tons kwa mwaka za yellow maize.

2) Watauza vifaranga na kununua kuku kwa wafugaji wadogo ambao watakuwa na ubora utakaoelekezwa hapo baadae. (Inategemewa kuku mmoja atakuwa na 1.5kg - 2 kg ambaye anakuzwa kwa siku 36 na kufika 2kg kwa kulishwa chakula maalum )


3) Wafungua maduka madogo(grocery) kwa ajili ya kuuza kuku ha ho yatakayomilikiwa na wazawa ambayo yataendeshwa kwa ubora wao na kwa arrangements watakazoeleza hapo baadae.


Hadi sasa wamekwishafungua unit 2 kati ya 24 zitakazojengwa ambayo kila unit ina hatchery 2, 1 ikiwa na kuku 13,000 kwa ajili ya mbegu na 1 kuku 74,000 wa nyama na mayai, zote zikiwa full automated 


changamkia fursa, kama kulima mahidi ya njano maana utakuwa na uhakika na soko. panga kutembelea eneo la mradi upate kujifunza zaidi.

1 comment:

  1. link, na contacts za hiyo fursa mkuu...tunafikaje hapo

    ReplyDelete