Fuatana nami katika kujifunza jinsi unavyoweza badili kutoka kulima mpunga kimazoe kwenda katika kilimo chenye kutoka mavuno tele kwa
mbinu za karne ya 21. Kilimo shadidi (System of rice intensification).
mbinu za karne ya 21. Kilimo shadidi (System of rice intensification).
HISORIA YA KILIMO SHADIDI (SRI) CHA MPUNGA
KILIMO SHADIDI ( SRI) ILIPOVUNJA REKODI YA DUNIA KWA MARA YA KWANZA.
Rekodi ya uzalishaji wa mpunga duniani haishikwi na Vyuo vya utafiti wa kilimo, wala wakulima wakubwa marekani. Ni mkuma mmoja kutoka katika kijiji cha Darveshpura nchini india. Kwa kutumia kanuni hii alivunja rekodi ya dunia kwa kuzalisha tan 22.4 (magunia 224) kwa hekari moja rcordi iliyokuwa ikishikiliwa na mchina ni 19 tani (magunia 190 kwa heka). Wastani wa mavuno kwa dunia kwa kutumia SRI duniani ni tani 4 (magunia 40 kwa heka).
SIRI NA FAIDA ILIYOJIFICHA NYUMA YA KILIMO SHADIDI
- Punguza msongamano wa miche, Panda mche mmoja mmoja kwa nafasi ili mizizi na shina vipate nafasi ya kutosha kukua.
- Utumizi wa maji kidogo kwa kilimo cha umwagiliaji hivyo unaeza kutumia maji kwa shughuli nyingine
- Unaweza kupanda eneo kubwa kwa kutumia mbegu chache
- Mazao yatatoka mengi na ni vigumu kupata magonjwa (mara mbili zaidi ya njia ya kawaida)
- Njia hii inaboresha ardhi na palizi lake linaifanya ardhi iwe na rutubaz zaidi.
MAANDALIZI YA KITALU
panda mbegu zako vizuri katika kitalu kwa njia ya kawaida. Mbegu za kupanda kwa mfumo huu zinashauliwa kupandwa zikiwa bado ndogo zenye umri wa siku zisizozidi 8 hadi12. Pengine kwa kutaka kuharakisha zaidi, loweka mbegu zikiwa ndani ya mfuko wa sandarusi kwa saa 24, zitoe kisha ziache kwa siku moja na unyevu hadi zitakapoanza kutoa mizizi kisha upeleke wa kitalu.
UPANDWAJI WA MICHE SHAMBANI
Mche mmoja mmoja unapandwa kwa ubali wa 24 cm, au mraba mdogo wenye urefu na upana wa cm 24 au 30 katika kila kona ya mraba kama inavyoonekana hapa chini.
UPALILIAJI
Palizi ni Muhimu kuhakikisha unapata mazao mengi. Katika SRI palizi hufanywa kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho Paddy Weeder Machine. Vibarua watatu kwa kutumia kifaa hiki wanaweza kumaliza herkari moja kwa muda mfupi. Njia nyingine pia zaweza kutumika.
paddy weeder machine.
Palizi linafanyika siku kumi baada ya kupanda, na litafanyka
hadi mara nne kwa kipindi cha uhai wa mpunga.
Faida tatu za aina hii ya palizi
- 1. Kwanza kifaa huki huzika majani katika udongo na kuwa mbolea (green manure)
- 2. Udogo husumbuliwa na kufanya hewa iingie ardhini, inafaida kwa mizizi na viumbe hai waboreshaji wa ardhi.
- 3. Kifaa hiki hukatakata mizizi ya mimea iliyo kandokando. Kitendo hiki huakikisha mizizi mipya inakua na yenye uwezo mkubwa wa kujitafutia chakula na madini ardhini.
UMWAGILIAJI
Unamwagilia, ardhi ikiisha lowana unafungulia maji.
Unaliacha shamba hadi litakapo kauna na ardhi kuanza kupasuka, hapo unamwagilia
tena na kufungulia maji kicha unaacha
likauke tena hadi ardhi ianze kupasuka tena. Mzunnguko huu unaweza kufanyika
kila baada ya siku saba hadi mmea utakapoanza kuzaa.
FAIDA YA MFUMO HUU WA UMWAGILIAJI
1.
Wadudu na bakteria wenye manufaa wanapata fursa
ya kurutubisha udogo na kufanya rdhi iwe yenye kufaa Zaidi.
2.
Unasidia kuokoa maji amabyo yanaweza kutumika
katika matumizi mengine ya shamba.
Ni kilimo safi na bora kwa mkulima anayetaka mabadiliko ya kianalojia
ReplyDelete