Karakana ya MkulimaUnapoamua kuingia katika kilimo, unapaswa kuruhusu kujua vitu vingi. Watu wengi tumeamua kuwa wakulima kama sehemu ya kupata pesa na kisha kukimbia kwenye shughuli nyingine. Hii imepelekea kuwepo na mafuriko ya watu wengi
mijini kukimbilia vijinini kukodi mashamba kulima kuvuna na kukimbia.

Wenzetu waliotambua kilimo kama fursa ya kudumu wao wameenda mbali zaidi. Shamba sio kitu cha kukodi tu bali ni vizuri ukamiliki shamba lako kisha ukapanga malengo makubwa.

Kwa kuwa sio utamaduni wetu kujua vitu vya kiufundi, tukiwa na nadharia ya kuwa ufundi ni taaluma ya mtu fulani. Hii imetusababishia kupuuzia vitu ambavyo wenda vingetupunguzia gharama.

Unapoamua kuwa na shamba ambalo lina mifugo, mazao mbalimbali, mashine za kuboresha mazao, na vitu vingi vya kilimo, inashauriwa upange kuwa na karakana pia.

Kama mkulima wa kilimo mchanyato au mchanganyiko , huwezi kukosa Treckta, Haevester, Chainsaw, Posho Mills, Madawa,packing tools  mashine nyingi za kufanyia kazi.

Huna haja ya kupiga simu mara kwa mara au kupeleka mashine zako kwa fundi. Panga kuwa na Karakana yako, ikiwezekana ukawa ukajifunza baadhi ya ujuzi mdogo mdogo wa kiufundi. Kama ni ngumu unauwezo wa kumleta fundi kwako kwa gharama nafuu.

Kwa mkulima mwenye malengo makubwa na ya muda mlefu  kuwa na karakana katika shamba lake
ni kitu cha kupewa umuhimu wa hali yajuu.

Makala ijayo, Tutajifunza karakana ya mkulima mdogo inapaswa kuwa na vitu gani vya muhimu.

No comments:

Post a Comment