KUPOTEZA SIO MWISHO WA KUTAFUTA: KUTOKA ZIMBABWE HADI MSUMBIJI





Walowezi wengi waliokuwa wanaishi zimbabwe, walidhni miaka yote watabaki hapo. Lakin wengi waliishia kulia na kukosa cha kufanya walipoona mashamba yao yakigawiwa kwa wazawa. Mashamba ambayo waliyaangaikia kwa gharama kubwa.

Bill Creswell, miaka 58 ni miongoni mwa walionyanganywa mashamba zimbabwe. yeye na wenzake waliamua
kutafuta fursa nchi jirani ya msumbiji. Alikwa hajawahi kutoka zimbabwe tangu kuzaliwa. Nchi aliyokuwa anaijua ni Zimbabwe tu.

MAlango mmoja ukifungwa usilazimishe, jaribu mwingine. Anasema aliingia msumbiji akiwa na begi la nguo tu. Lakini leo anamiliki shamba katika mji wa kilimo wa Chamaio.Anamiaka kumi tangu aondoke zimbambwe.

Chamalio ni mji ambao upo kilometa 95 kutoka Zimbabwe, Yeye na wenzake walianza kwa kukata majani na kufyeka shamba. Palivutia sio kwa sababu ya uwepo wa maeneo ya kukodi au hali nzuri ya hewa, lakini mkopo uliokuwa unatolewa na kampuni ya tumbaku ilikuwa ndio mlango sahihi wa kumtoa kimaisha huyu ndugu.

Tukio la kunyang'nywa mashamba liliwafanya wengi kukata tamaa, wengine wakchukia kilimo na kukimbilia australia lakini wachache walijitoa muanga na kutafuta fursa sehemu nyingine.

waliingia kijijini kijiji kikiwa kimelala. Leo mkulima mmoja anaajili wanakijiji hadi 200. Sasa analima mazao ya bustani, mbogamboga na hajutii uamuzi aliouchukua

No comments:

Post a Comment