KILIMO CHA TANGAWIZI






Kwa ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawiz zinastawi.

KUANDAA SHAMBA

Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA

Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia  mbolea ya mboji au samadi na usitumie  mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara  Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA

Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

KUVUNA

Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
 Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka

 Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawiz unaweza kusubir soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka

 Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzĂ lisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata  uzoefu kupitia hapo na kujua kama  eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawiz.

 Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg.
 Usikatishe tamaa pale  tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka

 HALI YA HEWA

Mimea hii husitawi katika maeneo  yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota

Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo

Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.

THANKS: UJASILIAMALI FORUM GROUP

28 comments:

  1. asante kwa msaada wako , maana umenipa elimu nzuri,mimi ni mkulima mdogo ndio nataka nijikite kwenye kilimo cha tangawizi.
    na kwa akili zangu za haraka haraka niliwaza same ninunue 200kg nikaoteshe kwa ajili ya kupata eneo kubwa, maana mbegu zake ni gharamaa
    nitarudi kwa mrejesho.

    ReplyDelete
  2. Karibu sana Eddy tuko pamoja, kama nawe unakitu unataka kutushirikisha tutumie email at miradikwanza@gmail.com, Asante.

    ReplyDelete
  3. Thanx alot its good deal.......ntapenda kuwasilana zaidi na kupata elim zaid email yangu ni ezzyelly@gmail.com plz naomba mawasiliano yako kwa maelezo zaidi ikiwzekana namba za simu....

    ReplyDelete
  4. Assure Santa kwa Elihu us kilimo nimekuelewa Sana kubwa ni kuyafanyia kazi.

    ReplyDelete
  5. Mikoa gani tangawiz inakubari na mbegu ya kg200 ni sh ngap na kg200 inaweza kupanda eka ngapi.my email
    mathiasmbwani@gmail.com

    ReplyDelete
  6. Mikoa gani tangawiz inakubari na mbegu ya kg200 ni sh ngap na kg200 inaweza kupanda eka ngapi.my email
    mathiasmbwani@gmail.com

    ReplyDelete
  7. Hata mim nahitaji kulima tangawizi nishapata shamba huko korogwe ila bado sijapata A-Z kuhusu tangawizi ndio napitia blog mbali mbali tushirikiane Kajirubaraka@gmail.com

    ReplyDelete
  8. Heka moja inaweza gharimu shingapu katika uzalishaji?

    ReplyDelete
  9. Naomba msaada zaid hasa kilimo cha tangawizi .maana nimepata maelezo tofauti na haya .
    Thanx

    ReplyDelete
  10. Kama unalima kanda ya kigoma mtaji m.5000000.

    ReplyDelete
  11. ni kampun gan inayouza mbegu ya tangawizi

    ReplyDelete
  12. hivi mkoa ambao wanalima sana tngawiz ni upi

    ReplyDelete
  13. nahitaji kujua ni mikoa ipi tangawizi inalimwa kwa wingi na pia napenda kujua gharama za mbegu yake ni shilingi ngapi?please email me; jonaskupa55@gmail.com

    ReplyDelete
  14. Mbegu ni za kl200 ni kama she. Ngapi? Pia je zinapatikana wapi afu inaweza kutumia sh. Ngapi kwa heka 1

    ReplyDelete
  15. Somo zuri sana japo upatikanaji wa mbegu na bei zake hujatueleza

    ReplyDelete
  16. Somo zuri sana japo upatikanaji wa mbegu na bei zake hujatueleza

    ReplyDelete
  17. Je kwa mwanza mbegu za tangawizi naweza kuzipata wapi?

    ReplyDelete
  18. Nataka nijue, hizo mbegu za kilo 200 kwa heka moja Ni Bei gani? Na unazipata wapi?

    ReplyDelete
  19. Nataka nijue hizo mbegu za kilo 200 kwa heka unapata wapi na sh ngapi? Email me please nurudiwe@gmail.com

    ReplyDelete
  20. Jamani unaambiwa kilo moja ni kati ya sh 1500/= hadi sh 6000/= cha msingi ni kupiga calculation, labda cha msingi kujua kilo 200 zinaweza tosha ekari ngapi?

    ReplyDelete
  21. Asante kwa darasa,nimejifunza somo kubwa Sana

    ReplyDelete
  22. Dah kilimo iki gharama jaman Yan pesa Zina Ni toka tu

    ReplyDelete
  23. Nimevutiwa xana na kilimo cha tangawizi ila kwa sasa nipo kigoma nataka niende nikajaribu kulima katavi

    ReplyDelete
  24. Nimevutiwa xana na kilimo cha tangawizi ila kwa sasa nipo kigoma nataka niende nikajaribu kulima katavi

    ReplyDelete
  25. Anaehitaji tangawizi mda wowote sehemu yoyote imufikie kiasi chochote
    Mawasiliano 0738317905

    ReplyDelete