Wa kwanza Afrika: kenya yajiandaa kunufaika na mkutano wa World Trade Organization (WTO)



Mkutano wa kibiashara (WTO) utakaoshirikisha zaidi wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 161  ambao ni  zaidi ya washiriki 5000 unatarajiwa kufanyika katika
jiji la Nairobi  mwishoni mwa mwaka huu. Kwa mara ya kwanza mkutano huu unafanyika  Afrika baada ya nchi ya uturuki kuiachia kenya hiyo nafasi.

Mkutano huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za kimarekani millioni nane.

Kenya inategemea kunufaika katika sekta ya Mahoteli, usafilishaji kama taxi pamoja na sehemu za malazi.

kwa sababu moja ya changamoto ya WTO ilikuwa ni kutotilia mkazo kwa nchi zinazoendelea, hiyo  ni ishara kwamba kutakuwa na faida kuwa kiuchumi na kimaendeleo kwa mkutano huu kupangwa Afrika.


Hii pia inaweza kuwa fursa kwa wadau mbali mbali wa afrika mashariki maana kila wanapokutana wafanyabiashara na wadau wa biashara huwa hakikosekani kitu cha kujifunza au kunufaika ukizingatia huu ni mkutano wa kwanza kufanyika afrika.








No comments:

Post a Comment