Ufanye nini unapoona ubunifu umekwama, Mambo MATANO



Unafanyaje pale unapoona unakwama, kila unachojaribu kufikiri kinagoma, wakati unaona ubunifu unagota. Unafanya kazi zako unafikia hatua unaona
hauna hamu kabisa ya kuendelea. Ufanyeje?

Wapo wataojilazimisha kwa nguvu na kuendela japo sio mara zote utafanikiwa na kuna uwezekano mkubwa ukawa unapoteza muda bure. Sio peke yako hali hii inamkuba karibu kila mtu.

Mwanasayansi Nguli Nikola Tesla, Baba wa umeme, Mota Mwasiliano na Uvumbuzi wake umepelekea kubadili dunia ya ya teknolojia juu chini. Pamoja na uwezo mkubwa aliojaaliwa nao Mara nyingi alifikia kipindi katka maabara yake ya kujaribia anakwama kufikiri, anachoka, haoni wazo jipya. Muda huu au hali hii yeye aliiondoa kwa kuwapigia simu marafiki zake mfano Mark Twain na kujadili vitu vingine tofauti kabisa. wakati mwingine alilala dakika kadhaa na kuamka akiwa yuko flesh. 

Yawezekana unafanya hivi lakini hauna uhakika kama ni sahihi. Hapa chini yapo mambo matano yatakayokusaidia ukiwa karika hali hii. Siri ni kwamba unapofanya kitu tofauti ambacho hakihitaji umakini wa hali ya juu, unakuwa unaurudisha ubongo katika hali ile ya kufikiri vizuri na kuwa katika mazingira ya kiubunifu zaidi.

1.Tafakari/Meditate:Kuwa katika hali ya kutofikiri chochote.unaweza kukaa kwenye kiti, weka umakini wako katika upumuaji, usiwaze chochote bali jinsi pumzi inavyotoka na unavyoivuta. Hii ni njia mojawapo ya meditation zipo nyingi. 

2.Fanya Zoezi:Jiingize katika shughuli zinazokufanya kupumzisha akili na njia hii mara nyingi ni kuelekeza umakini katika mazoezi. unaweza kuamua kutembeatembea kidogo aukunyoosha viungo kwa muda  baadae ukarudi kuendelea na shughuli.

3.Fanya kitu kingine cha kibunifu. Mfano wengine huamua kujishugulisha na utunzi wa nyimbo, Kujifunza shughuli mpya ya kiufundi, kipika chakula kipya cha tofauti, au kujifunza kutumia kifaa kipya cha mziki kama kinanda, gitaa au firimbi. kikubwa ni kujishugulisha na kitu kipya tofauti na ulichokuwa unafanya.

4.Soma kitu chochote:Soma kitu chochote ambacho haina uhusiano na jambo unalofanya.
soma gazeti, pitia habari zisizokuchosha sana au chochote kile ambacho kitakuamisha mawazo juu ya tatizo lililoleta mkwamo. 

5. Kubali Kusinzia kwa dakika chache/ TAKE A NAP. Weka alarm kwenye simu yako kwa dakika chache. Acha unachofanya. Sinzia muda mfupi ili kupumzisha akili. au haupo katika hali ya kupata usigizi mfupi au meditation. Acha unachofanya kaa pembeni bila kufanya chochote.


miradi kwanza



No comments:

Post a Comment