Application 6 katika SIMU yako zinazoweza kukusaidia ewe mkulima wa leo

IMG_5271



Zipo sababu nyingi zinazoshangaza kwa nini hadi leo wewe mkulima usipange kumiliki simu ya kisasa yenye uwezo wa kukuweka karibu na wenzako sehemu mbalimbali duniani. Leo hii kuna taarifa nyingi
zinakupita wenda ungejua usingekuwa hapo kibishara yako ya kilimo. Vijana husuani ambao wameingia katika kilimo. Ni wakati sasa kufanya mambo kidigitali zaidi.

Kwa tanzania kuna magroup lukuki ya kilimo na ufugaji wassap, Telegram, facebook n.k , usikubali kuishi kama kisiwa kutana na wenzako uweze kujadili fursa, changamoto na mbinu mbalimbali za kilimo. magroup haya yapo kitaifa na hata kimataifa.

Vodacom tanzania wanatoa taarifa ya kilimo na masoko kupitia mtandao wa simu. Usikupali kupitwa na fursa hii pia.

Hapa chini ninakuorodheshea Application za wenzetu ambazo unaweza kuongeza katika smartphone yako ukafaidika na taarifa mbalimbali za kilimo. Nyingi ya application hizi zinatumiwa marekani lakini wewe mkulima wa tanzania au afrika mashariki imefika wakati tuanze kuwaza kimataifa na kujua wenzetu wanafanyaje katika kilimo.

1. NCGA Action 
hii application ilitengenezwa rasmi ili kuwajulisha wakulima wa mahindi nini kinachoendelea katika miji mikubwa marekani hususani washington D.C ambayo yanaweza kuathili wakulima kwa njia tofauti.
Kuna taarifa nyingi zinazoweza kukusaidia mkulima kuanzia kupanda na kuvuna. Unaweza kuidownload na kutumia.

inapatikana kwa simu za Android na Apple pia

2. Seed Finder
Hii inapatikana kwa Farmers Business Network Membeship.
Utapata taarifa za kiuhalisia kuhusu mbege aina tofautitofauti zaidi ya 550. Kwa mkulima wa afica mashaiki kijana pia unaweza kupata taarifa zitakazokusaidia katika application hii.

inpatikana kwa simu za apple

3.KSUSoyYieldCalc 
Hii ni adnroid apllication. Unaiweka katika simu au notepad yako. Itakusaidia ewe mkulima wa soya kujua utapata mazao kiasi gani. Kwa kujaza baadhi ya kitu vya muhumi nayo inakupa makadilio ya mazao utakayopata.

4.MachineryGuide
Hii inawasaidia wakulima kubadili simu zao kuwa kifaa kidogo cha GPS (utahitaji kununua software na antenna).zinatumika nchi za ulaya lakini unaweza fuatilia link hapo chini kuona ni kwa jinsi gani inaweza kukupa tija katika shughuli zako za kilimo.
http://www.machineryguideapp.com/en.

5.Farm at Hand
Hii inapatikana katika Android na apple pia.
kwa wenzetu wanaitumia kupata taarifa mbalimbali kuanzia kupanda hadi mavuno. Pia kama unatumia mashine au matractor kuna taarika unajaza inakusaidia kujua hata ni muda gani wa kufanya matengenezo ya mashine zako na taarifa nyingine zitakazo kusaidia hata wewe kijana wa afrika mashariki. Download fuatilia na uone kipi kinakufaa.

6:Farm Radio
Farm Journal Media wameanzisa Farm radio inayotoa taarifa mbalimbali za kilimo, jinsi ya kutunza shamba na taarifa mbalimbali za kilimo. Hii inaweza kukusaidia ewe mkulima au mpenzi wa kilimo unaishi markani na unahitaji kuja kuanzisha kilimo huku, naamini unaweza kupata taarifa zitakazo kufanya kuwa bora zaidi. Hata tulio huku bado tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea.

Simu tulizo naozo hususan SMARTPHONES, Zinaweza kuwa na manufaa zaidi kama tukizitumia katika shughuli za maendeleo pia. Wakulima wapo dunia nzima, ni wakati sasa tukubali kuvuka mipaka na kuaongalia wenzetu wanafanya nini duniani na kuchukua kinachowezekana kwetu.

miradikwanza


No comments:

Post a Comment